“Mechi bila mashabiki hazitofautishi ubora wa wachezaji” Beckenbauer

Mkongwe wa Bayern Munich Franz Beckenbauer amesema mechi kuchezwa bila mashabiki haziwezi kutofautisha ubora wa wachezaji.

Akiwa amebeba historia lukuki, mshindi huyo wa Kombe la Dunia na Kocha wa zamani alifika dimba la Allianz Arena kushuhudia mtanange huo kufuatia mwaliko wa Mkurugenzi wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge.

Hata hivyo ilipata kandanda safi baada ya kuona timu ya Bayern Munich ikiitandika Eintracht Frankfurt goli 5-2, ambapo kabla ya hapo ilikuwa 3-2.

Beckenbauer anasema kutazama mechi bila uwepo wa mashabiki hasa kwa soka la Ujerumani lenye utamaduni wa mashabiki kujaa viwanjani inahuzunisha, ingawa hakusita kusema amefurahia kutazama mechi hiyo.

Ligi ya Bundesliga ikiwa ni kandanda ya kwanza kubwa kuanza kuchezeka baada ya janga la virusi vya Corona inaonekana mambo yanawaendea vizuri hata tamati, Beckenbauer ameongeza kwa kusema amefurahia kurudi kwa ligi.

“Hakuna shabiki anayefurahia michezo hii kuchezwa bila uwepo wake, na kwa sababu hawajaruhusiwa wanalazimika kukaa majumbani, hilo ni jambo ngumu kwao”,

Shida ya kucheza bila mashabiki inakuwa vigumu kutofautisha viwango vya wachezaji wote unaweza kuwaona sawa”. Aliongeza ligendi huyo mwenye heshima kubwa katika soka la Ujerumani.

Akizungumzia ujio wake baada ya mchezo kocha wa Bayern Munich Hansi Flick alisema “nimefurahi kumuona akitazama mchezo, bila shaka amependezwa na namna tumecheza siku ya leo, na atakuwa anakuja siku nyingine kama leo” alisema Flick.

Mchezo ujao wa Bayern Munich utakuwa dhidi ya Borrusia Dortmund Jumanne usiku wa Mei 27.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends