Mechi nne EPL kumpa ubingwa Man City, washinda 2-0 kwa Leicester City

Vinara wa Ligi Kuu England klabu ya Manchester City wanahitaji ushindi wa mechi nne pekee kubeba taji la EPL baada ya kuifunga timu iliyo nafasi ya tatu Leicester City bao 2-0 mchezo wa Leo Jumamosi Aprili 3.

Goli la kwanza kwa Manchester City ambao watakuwa wanamuaga nyota wa timu hiyo Sergio Kun Aguero limefungwa na Benjamin Mendy dakika ya 58, kabla ya Gabriel Jesus kuongeza la pili na kufuta uwezekano wa ushindi kwa vijana wa Rodgers.

City wako na faida ya alama 17 kwa timu iliyo nafasi ya pili Manchester United ambayo kesho Jumapili itacheza dhidi ya Brighton ambapo wamefikisha pointi 74 zikiwa zimebakia mechi saba.

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anahitaji alama 11 kutoka kwenye mechi hizo.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares