Mechi ya AFCON kati ya Ghana na Kenya kuchezwa Ohene

Shirikisho la Soka barani Afrika CAF, limetangaza kuwa mechi ya mwisho kufuzu katika fainali ya mataifa bingwa barani Afrika mwezi Juni nchini Misri, kati ya Black Stars ya Ghana na Harambee Stars ya Kenya, itachezwa katika uwanja wa Ohene jijini Accra.

Ghana ambao wameshinda taji la Afrika mara nne, walipoteza mechi ya kwanza, jijini Nairobi bao 1-0 mwezi Septemba mwaka uliopita.

Black Stars, haijawahi kucheza katika uwanja wa Kimataifa wa Accra baada ya kuishinda Mauritania mabao 7-1 katika mechi ya kufuzu kucheza fainali za bara Afrika mwaka 2017. Mechi hiyo itachezwa tarehe 23 mwezi huu.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends