Mechi ya kibabe mno, Marseille, Paris St-Germain zatoshana nguvu

Ukisikia mechi ya dabi basi ndiyo hii. Mechi ikipigwa kidabi haswa, wachezaji wakicheza katika hali ya hatari kiusalama wao.

Dakika 90 zikimalizika kwa sare tasa, ni mechi ya Marseille dhidi ya Paris St-Germain kufuatia matukio ya VAR huku mashabiki wakiingilia mchezo mara kadhaa.
Kutokana na mashabiki kurusha chupa, wakati Neymar akipiga kona walinzi walilazimika kumzunguka nyota huyo muda wote akiwa anapiga mpira wakutenga.
Ungwe ya pili, shabiki alivamia uwanjani na kumshika Lionel Messi tukio ambalo Maaskari walilazimika kuingia tena uwanjani.
Matumizi ya var yakionekana machungu kwa kila upande baada ya goli kukataliwa huku beki wa kulia Hakimi Achraf akitolewa nje ya uwanja kufuatia kuonyeshwa kadi nyekundu akicheza faulo bora kwa Cengiz Under.
PSG, bado wanaendelea kushikilia rekodi ya kutopoteza mchezo wowote katika mechi 11 msimu huu akiwa na alama saba tofauti kileleni.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends