Mechi ya kisasi: Liverpool dhidi ya Arsenal

Mechi yenye kisasi. Mechi ambayo hutazamwa na wachezaji wakubwa kina Mohamed Salah na Pierre Emerick Aubameyang kama sehemu ya kutengeneza historia yao. Mechi za namna hii huvutia kuanzia watazamaji wengi, mawakala wengi huenda ikawa njia ya kutokea kwa wachezaji wadogo. Kizuri kuliko vyote ni mechi ambayo huwa inaruhusu magoli ya kutosha kwa pande zote mbili.

Ni Liverpool dhidi ya Arsenal katika mechi ya EPL ndani ya dimba la Anfield 19:30.

Timu hizi zinakutana kipindi ambacho zote zinaonekana kuwa na ubora ulio sawa, Arsenal ameshinda mechi mbili za awali EPL hali kadhalika kwa Liverpool.

Arsenal wanacheza soka nzuri, ni washindani huku wachezaji wapya wakiwa wameongeza pilipili kwenye kachumbari iliyotengenezwa vyema.

Tangu msimu uliopita Liverpool ni kachumbari kamili, hii inaongeza radha ya mchezo huo maradufu.

Hapa Amani Sports News inakuletea wachezaji waliotengeneza majina kupitia mchezo huo kwa kufunga goli

Thierry Henry 

Ni nguli wa Arsenal, pengine hutajwa kama mchezaji bora zaidi katika kizazi cha miaka 15 ya hivi karibuni. Kwenye mchezo baina ya Arsenal na Liverpool amefunga goli 9 katika mechi 18. Alikuwa sehemu ya kikosi kilichocheza bila kushindwa 2003/04.

Andrey Arshavin

Hakuwa staa hata! Alikuwa mchezaji muhimu kwenye matukio muhimu. Anakumbukwa kwa kufunga goli 4 kwenye sare ya goli 4-4 mwaka 2009.

Martin Sekrtel

Pengine umeshitushwa na jina hili la mlinzi wa Liverpool kutokana na rekodi yake ya kujifunga lakini beki huyo aligeuka nuru kwenye matokeo ya 5-1, akifunga goli 3 na kuwa Hat trick yake ya kwanza katika soka lake.

Robert Firmino

Katika kizazi hiki cha sasa, mashabiki wa Arsenal wasingependa kumuona Mbrazil Firmino akiongoza mshambulizi ya Liverpool chini ya Klopp. Amehusika kwenye goli 8 na kumshika Fowler. Mbali na kufunga amekuwa na wastani mzuri wa kutengeneza nafasi kwa wachezaji wenzake.

Robin Van Persie

Kabla ya miezi mitano kujiunga na Manchester United, Van Persie alifunga goli bora sana ambalo hutajwa kama goli bora katika maisha ya staa huyo. Kama ilivyo kwa Roberto Firmino, Robin amefunga goli 8.

Wachezaji wengine ambao wamewahi ama hutamba kwenye mchezo wa Liverpool dhidi ya Arsenal ni pamoja na Sadio Mane na Peter Crouch.

Hawa ni baadhi ya wachezaji waliowahi kutamba katika mechi hii, lakini pia kuna mastaa wanaotamani kuendelelea kutengeneza historia kupitia mtanange huo miongoni mwao ni Pierre Emerick Aubameyang, Mohamed Salah, Lacazette, Virgil Van Dijk na wengine.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends