Mechi ya Simba, Polisi Tanzania yaota mbawa

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara imesema mchezo wa Ligi Kuu Bara baina ya Simba na Polisi Tanzania uliotarajiwa kuchezwa Oktoba 20, 2021 sasa unatarajiwa kuchezwa Oktoba 27 mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB) kupitia kwa Afisa Habari wa bodi hiyo Karim Boimanda imeeleza kuwa sababu kubwa ya kuota mbawa kwa mtanange huo ni simba kuwa ni ratiba ya michuano ya kimataifa.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, klabu ya Simba itakutana na changamoto ya usafiri kutoka Botswana kurudi nchini mapema na kucheza mechi ya Ligi, baada ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy Fc mtanange utakaopigwa Octoba 17 Jumapili.

Kufuatia mabadiliko hayo, mechi hiyo ya Ligi itachezwa muda ule ule wa saa moja usiku katika dimba la Benjamin William Mkapa.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends