Mechi yaahirishwa baada ya Payet kupigwa na chupa uwanjani

Mchezo wa Ligi Kuu nchini Ufaransa Ligue 1 baina ya Lyon na Marseille umeahirishwa kufuatia kiungo mshambuliaji wa zamani wa West Ham United na timu ya taifa ya Ufaransa Dimitri Payet kupigwa na chupa iliyokuwa imerushwa na shabiki mmoja.

Payet alipigwa na chupa wakati akijiandaa kwenda kupiga mpira wa kona dakika tano baada ya kuanza kwa mchezo huo, baada ya tukio hilo refarii Ruddy Buquet aliwaruhusu wachezaji kutoka uwanjani.

Wakati akitoka uwanjani kiungo huyo wa Marseille alionekana akiugulia maumivu huku akishikilia barafu sehemu ya juu ya jicho.

Mchezo huo uliahirishwa mapema mpaka sasa haujachezwa tena, na hakuna taarifa yoyote.

Nchini Ufaransa kumekuwa na matukio kama hayo yenye kujirudia, itakumbukwa mwezi Agosti timu ya Nice ilikatwa alama mbili kwenye mechi dhidi ya Marseille huku Payet akifungiwa mechi mbili baada ya kurudisha chupa aliyokuwa amepigiwa na kusababisha vurugu zaidi kwa mashabiki.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends