Mechi za EPL kuonyeshwa bure, muda wa mechi pia kubadilika

Ligi Kuu ya England wamefanya kikao cha kujadili uwezekano wa kubadilisha muda utakaotumika kucheza mechi sawa na mpango wa kuonyesha baadhi ya mechi bure.

Katika mpango wa kurejesha ligi, wamekusudia ligi kuanza kuchezwa Juni ili kutoa mwanga zaidi ya kumalizika kwa michuano ya klabu bingwa na ligi ya Europa.

EPL katika kikao chao wameendelea na mazungumzo na wenye miliki ya kuonyesha michezo, serikali, na vilabu juu ya kuonyesha baadhi ya michezo bure kwenye akaunti ya mtandao wa YouTube wa vilabu husika.

Mechi 92 zimesalia kutamatisha kandanda ya ya EPL lakini michezo 47 huenda zikaonyeshwa kati ya Sky au BT kwa malipo, wakati mechi 45 zinazosalia zinapangwa kuonyeshwa bure kwa njia ya YouTube.

“Haitakuwa na maana yoyote kama michezo ya EPL itachezwa bila mashabiki halafu isionyeshwe kwa jamhuri” alisema Oliver Dowden.

Mabadiliko ya ratiba ya muda kuchezwa pia ilijadiliwa Ijumaa katika kikao cha wadau mbalimbali ambapo Aprili Uefa waliweka muda wa mechi za Jumamosi kufanyika kuanzia saa 11 jioni ili kujinusuru kuangukia katika janga la virusi vya Corona.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends