Mechi za mwisho kufuzu AFCON kukamilika mwezi huu

55

Michuano ya mwisho, hatua ya makundi, kuwania fainali ya michuano ya soka barani Afrika, itakayofanyika mwezi Juni nchini Misri, itachezwa tarehe 22 mwezi huu.

Makocha mbalimbali wameanza kutaja vikosi vya wachezaji kuanza maandalizi. Tanzania itacheza na Uganda katika mechi muhimu jijini Dar es Salaam na tayari kocha, Mnigeria Emmanuel Amunike amekitaja kikosi kuanza maandalizi hayo.

Kenya itakuwa jijini Accra kucheza na Ghana, timu zite zimeshafuzu. Burundi itakuwa jijini Bujumbura kutafuta ushindi muhimu dhidi ya Gabon.

DRC nayo itakuwa jijini Kinshasa kucheza na Liberia kutafuta ushindi.

Author: Bruce Amani