Medo asema Sofapaka ina uwezo wa kutwaa KPL

Siku mbili tu baada ya kuteuliwa kuwa kocha mkuu wa Sofapaka, Mmarekani Melis Medo anasema klabu hiyo unao uwezo mkubwa wa kulitwaa taji la ligi kuu nchini Kenya KPL.

Anasema wachezaji waliomo klabuni humo wana uzoefu wa kutosha kushiriki michuano ya Kenya na kupata yanayohitajika.

Aidha anasema hadhani kuwa kwa sasa anahitaji kuongeza wachezaji wengine japo hajawaelewa vya kutosha vijana alionao ili kuutathmini ipasavyo uwezo wao. Sofapaka mara ya mwisho kulitwaa taji la Kenya ilikua mwaka wa 2009.

Medo alikuwa akiinoa Nakumatt FC ambayo sasa inafahamika kama Mount Kenya United na alisaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya “Batoto Ba Mungu” Sofapaka.

Author: Bruce Amani