Messi afunga lakini Barcelona yabanwa mbavu na Cadiz katika sare ya goli 1-1

Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Lionel Messi amefunga goli katika mchezo wa historia katika maisha yake baada ya kufikisha mechi 506 ndani ya La Liga ingawa Barcelona imeendeleza kuchechemea baada ya kutoa sare ya bao 1-1 na Cadiz.

Barca ambao wametoka kuchapwa goli 4-1 dhidi ya Paris St-Germain katikati ya wiki katika Ligi ya Mabingwa, walikuwa wanahitaji ushindi ili kurudisha hali ya kujiamini lakini haikuwa hivyo.

Messi alifunga goli la kwanza kwa penati kabla ya Cadiz kusawazisha bao hilo kupitia kwa Alex Fernandez ambalo lilikuwa shuti lao la kwanza ambalo lililenga goli na kuzaa bao hilo.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares