Messi aisaidia Barcelona kupambana katika sare na Valencia

Walihitaji umahiri wa Lionel Messi ili kuepuka kichapo na watamshukuru kuwa kuwasaidia kupata angalau pointi moja. Messi alifunga mabao mawili wakati Barcelona ilitoka nyuma 2 – 0  na kutoka sare nyumbani dhisi ya Valencia katika matanange mkali sana wa La Liga.

Kevin Gameiro alifunga bao la ufunguzi kwa upande wa wageni Valencia, kabla ya Daniel Parejo kuongeza la pili kupitia mkwaju wa tuta.

Messi alifunga bao lake la kwanza kupitia penalty, na la pili likawa mkwaju aliopiga kutoka pembeni mwa kisanduku cha hatari katika dakika ya 64.

Atletico Madrid watacheza dhidi ya Real Betis Jumapili, wakilenga kupunguza kabisa pengo dhidi ya vinara Barcelona hadi pointi tatu.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends