Messi apiga hat trick wakati Barca ikiizamisha Celta Vigo

Lionel Messi alifunga hat trick nyingine Jumamosi na kuiongoza Barcelona katika ushindi wa 4 – 1 dhidi ya Celta Vigo na kumpunguzia shinikizo kocha Ernesto Valverde.

Messi alifunga penalty na kisha free kicks mbili katika vipindi vyote viwili vya mchezo baada ya Lucas Olaza kuisawazishia kwa muda mfupi Celta kwa kuchonga free kick yak wake uwanjani Camp Nou. Sergio Ramos alikamilisha ushindi huo kwa upande wa Catalans.

Hiyo ni hat trick ya 34 ya Messi ambayo inamuweka kwenye idadi sawa na Cristiano Ronaldo, na ushindi huo unaiweka Barca kileleni mwa La Liga juu ya Real Madrid kwa faida ya mabao

Madrid walishikilia usukani kwa muda baada ya kuibamiza Eibar 4 – 0 mechi ambayo Karim Benzema alifunga mabao mawili na Eden Hazard akawa moto wa kuotea mbali.

Author: Bruce Amani