Messi arejea dimbani kuivaa Dortmund Ligi ya Mabingwa

Lionel Messi amerudi kwenye kikosi cha Barcelona kuelekea kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa ulaya dhidi ya Borussia Dortmund siku ya Jumanne.
Nahodha huyo raia wa Argentina, mara ya mwisho alicheza mwezi mei mwaka huu, Mashindano ya Copa America
Messi ameruhusiwa na jopo la madaktari siku ya Jumatatu na kujumuika na wenzake.
Kwenye mechi za La Liga, Barcelona bila Messi wameshinda mechi mbili kati ya nne na kupoteza mechi moja.
Pia ndani ya kikosi hicho Ansu Fati, 16, amejumuishwa kuwa sehemu ya kikosi kinachojiandaa na mchezo wa Ligi ya mabingwa

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends