Messi awabwaga Ronaldo na van Dijk tuzo ya mchezaji bora

351
Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa kiume wa mwaka tuzo ilitolewa Jijini Milan Italia na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) huku strika wa Juventus Cristiano Ronaldo na mlinzi wa Liverpool Virgil van Dijk wakikosa tuzo hiyo.
Inakuwa tuzo ya sita kwa Messi baada ya kutwaa tuzo kama hiyo pia mwaka 2009, 2010, 2011, 2012 na 2015.
Strika huyo raia wa Argentina mwenye miaka 32 aliisaidia Barcelona kuchukua ubingwa wa La Liga na kufika nafasi ya nusu fainali ya Ligi ya mabingwa wakitolewa na Liverpool.
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Marekani Megan Rapinoe ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka upande wa Wanawake.
Lionel Messi alifunga goli 54 kwenye michezo 58 kwenye ngazi ya klabu na timu ya taifa msimu wa 2018/2019 wakati Cristiano Ronaldo, akifunga mabao 31 ndani ya michezo 47.
KLOPP AWAPIGA CHINI GUARDIOLA NA POCHETTINO
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp ametajwa kuwa kocha bora wa mwaka kwa Wanaume akiwashinda makocha wawili Pep Guardiola na Mauricio Pochettino.
Tuzo hiyo inakuja baada ya kuifikisha Liverpool nafasi ya pili ya EPL wakiwa na alama 97 nyuma ya Manchester City na kuchukua ubingwa wa Uefa wakiifunga Tottenham goli 2-0.

Author: Bruce Amani