Messi ndiye mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani

Mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi ndio anayelipwa malipo ya juu zaidi kuliko wachezaji wote duniani, alilipwa dola milioni 127 katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, kwa mujibu wa orodha ya jarida la Forbes ya wachezaji 100 wanaolipwa vizuri.

Mshambuliaji wa Juventus, Mreno Cristiano Ronaldo anashikilia nafasi ya pili akilipwa dola milioni 109, huku mshambuliaji wa Paris Saint Germain Neymar ambaye ni raia wa Brazil akiwa katika nafasi ya tatu kwa malipo ya dola milioni 105.

Mwaka jana mchezaji aliyelipwa kuliko wote duniani alikuwa ni mwanamasumbwi Floyd Mayweather, lakini sasa ameshuka katika orodha hiyo.

Mchezaji wa tenis Mmarekani Serena Williams ni mwanamke pekee katika watu 100 , wanaolipwa vizuri, na kwa mujibu wa Forbes analipwa dola milioni 29.2

Mshindi wa mara tano wa mashindano ya dunia ya magari ya Formula 1 Lewis Hamilton na mshindi wa zamani wa masumbwi uzani wa juu Anthony Joshua ndio wanariadha wanaolipwa vizuri zaidi nchini Uingereza, wakichukua namba 13 na malipo ya dola milioni 55.

Messi ndie mchezaji pekee wa pili wa soka kuwa juu katika viwango baada ya Ronaldo, na ndiye mwanariadha wa nane pekee miongoni mwa wanariadha tofauti kuchukua namna moja tangu orodha hiyo ilipoanza kutolewa mnamo 1990.

Ni mara ya kwanza kwa mchezaji wa mpira wa miguu kuwekwa miongoni mwa watu watatu wanaolipwa vizuri kwa kucheza.

Mchezaji wa Manchester United Paul Pogba ndiye mchezaji anayelipwa zaidi katika primia Ligi, na katika orodha ya Forbes anashikilia nafasi ya 44t na malipo ya dola milioni 33. (£25.9m).

10 walio juu katika Orodha ya Forbes:

  1. Lionel Messi dola 127
  2. Cristiano Ronaldo dola 109
  3. Neymar dola milioni 105
  4. Canelo Alvarez dola milioni 94
  5. Roger Federer dola milioni 93.4
  6. Russell Wilson dola milioni 89.5
  7. Aaron Rodgers dola milioni 89.3
  8. LeBron James dola milioni 89
  9. Stephen Curry dola milioni 79.8
  10. Kevin Durant dola milioni 65.4

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends