Messi, Ronaldo kwenye orodha ya washindani wa tuzo ya UEFA

Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi na mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo wamechaguliwa kuingia kwenye kinyang’ anyiro cha kushinda tuzo ya UEFA msimu uliopita. Shirikisho la mpira barani Ulaya (UEFA) limetaja pia walinda mlango watakaogombania nafasi ya mshindi katika nafasi hiyo. Messi alifunga goli 12 msimu uliopita akishuhudia timu yake ikiondolewa hatua ya nusu fainali na waliokuw mabingwa msimu huo Liverpool kupitia magoli la Origi Divock.
Upande wa Ronaldo alifunga goli sita akiifikisha timu yake hatua ya robo fainali ya michuano hiyo inajumuisha goli tatu (Hatrick) dhidi ya Atletico Madrid, Juve ikipoteza mbele ya Ajax. Wachezaji hao wawili wanaungana na mshambuliaji wa Liverpool, Sadio Mane katika kipengele cha mshambuliaji bora huku Jordan Henderson, Christian Eriksen na Frenkie de Jong, wanagombani tuzo ya kiungo bora wa michuano hiyo. De Jong sio kiungo tena wa Ajax sasa yupo Fc Barcelona.
Nafasi ya ulinzi imetajwa kugombaniwa na walinzi watatu kinda wa Ajax Matthijs de Ligt, Virgil van Dijk na Trent Alexander-Arnold wote Liverpool. Liverpool, wakiwa mabingwa wa taji la Uefa 2018/19 wametoa mchezaji mwingine watatu nafasi ya golikipa ambaye ni Allison atashindana na walinda mlango kutoka Tottenham Hotspurs Hugo Lloris na Marc-Andre ter Stegen wa Barcelona. Tuzo za Uefa mwaka huu zitatolewa Agosti 29 mwaka huu mjini Monaco nchini Ufaransa wakati wa droo ya ratiba ya michuano mingine kwa msimu wa 2019/20.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends