Messi yupo yupo sana Barcelona, asaini hadi 2026

307

Lionel Messi amekubali kuongeza mkataba mpya wa kuendelea kukitumikia kikosi cha Barcelona mpaka mwaka 2026 huku akiwa amepunguza mshahara wake.

 

Messi, 34, ambaye mkataba wake ulimalizika mwezi uliopita Juni 30, imeelezwa kuwa pauni milioni 123 Barcelona imemlipa mchezaji huyo kubakia klabuni hapo.

 

Kwa sasa Messi yuko kwenye mapumziko baada ya kushinda ubingwa wa Copa America. Mkataba wake unakuja ikiwa ni miongoni mwa malengo ya Rais Juan Laporta aliyeahidi hivyo wakati wa kampeni zake.

 

Barca pia wana mpango wa kumtoa mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann kwenda Atletico Madrid ambapo Saul Niguez, anatajwa kutua viunga vya Camp Nou kubwa zaidi ni katika kupunguza gharama za malipo ya mishahara.

 

Messi amekuwa alikuwa anahusishwa kujiunga na Paris St-Germain na Manchester City kabla ya mkataba huo mpya lakini alikuwa anahusishwa kwenda Marekani katika Ligi ya MLS.

Author: Asifiwe Mbembela