Mfahamu kocha mpya wa Chelsea, Frank Lampard

Baada ya Chelsea kumtambulisha rasmi Frank Lampard kuwa kocha wao mpya kwa mkataba wa miaka mitatu, hapa chini Amani Sports News inakuleta kwa kifupi historia ya Lampard.

Frank Lampard alijiunga na Chelsea akitokea timu ya utotoni mwake ambapo pia Baba yake Frank Lampard Sr alichezea West Ham kwa ada ya paundi milioni 11 na ilikuwa ni mwaka 2001.

Akiwa Chelsea ameshinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Europa Ligi, alishinda mataji matatu ya Ligi kuu England (EPL), FA mara nne, na Kombe la Ligi mara 2.

Lampard anatajwa na Wachambuzi wengi wa masuala ya soka kama kiungo bora kuwahi kutokea katika zama zake, akisaidiwa na takwimu za kufumania nyavu kwani alifunga zaidi ya goli 10 kwa misimu 10 zaidi, pamoja na msaada wa magoli 111 jambo lisilo rahisi kwa wachezaji wengi.

Aidha, Lampard ndiye kinara wa mda wote katika kufumania nyavu ana goli 221 ambazo hazijafikiwa na mchezaji yeyote ndani ya The Blues.

Msimu wa 2004/05 hutajwa kama msimu bora kwa Frank Lampard ndani ya Chelsea baada ya kuisaidia timu hiyo kubeba taji kwa kufunga goli mbili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Bolton, huku akiwa amefunga goli 13 msimu huo.

Lampard aliachana na Chelsea Juni mwaka 2014, akajiunga na Manchester City, kabla ya kuachana nayo mwishoni mwa mwaka huo kisha akatimukia New York City ya Marekani mwaka 2015.

NGAZI YA TAIFA

Lampard hata timu ya taifa ya England alifanya vizuri katika enzi zake, akishirikiana na wakongwe wengine kama Wayne Rooney, John Terry, Steven Gerrard amecheza mechi 106 tangu mwaka 1999 akiwa amefunga jumla ya goli 29.

Frank James Lampard alishiriki mara tatu kwenye fainali za Kombe la Dunia na mara moja kwenye fainali za bingwa wa dunia ngazi ya klabu.

Alitundika rasmi daluga mwaka 2017 baada ya zaidi ya miaka 21 kuitumikia taaluma yake.

MAFANIKIO KAMA KOCHA

Lampard, 41, hana mafanikio makubwa kwenye soka kama kocha, hata umri wake unasadifu hilo. Kikubwa ambacho ameonyesha ni kufika fainali ya michezo ya mtoano kufuzu kucheza EPL akiwa na Derby Country mwaka 2019 licha ya kupoteza dhidi ya Aston Villa.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments