Mfumo wa mechi za nyumbani na ugenini kuendelea kama kawaida – CAF

601
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) litaendelea na utaratibu wake wa mechi zake kuchezwa nyumbani na ugenini kuanzia hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kuanzia mechi za msimu huu.
Endapo timu mbili kutoka nchi moja zitafuzu hatua ya fainali, nchi hiyo itajikatia tiketi ya moja kwa moja kuandaa mashindano hayo makubwa katika ngazi ya vilabu.
Kama matokeo ya kuingia hatua ya fainali yatakuwa hayahusishi timu kutoka nchi moja basi mfumo wa uwanja huru utaendelea kutumika kama kawaida.

Author: Asifiwe Mbembela