Micho atimuliwa kuinoa Chipolopolo ya Zambia

Shirikisho la Kandanda Zambia limefikia maamuzi ya kusitisha kandarasi ya kocha wa timu ya taifa ya Zambia Milutin Sredojevic “Micho” kufuatia matokeo mabovu ndani ya timu hiyo.

Rais wa Shirikisho hilo Andrew Kamanga, alisema maamuzi ni ya Shirikisho kwani ameshindwa kuifanya timu kuamka inazidi kudidimia kisoka.
Kocha huyo raia wa Serbian alipata nafasi ya kukinoa kikosi cha Chipolopolo mwezi Februari 2020 ambapo matumaini yalikuwa kuimarika kwa uchezaji wa timu kwenye Kombe la COSAFA lakini imekuwa tofauti hasa baada ya kufungwa na Lesotho na Switzerland.
Miezi 8 imesalia kwenye kandarasi yake kukamilisha mkataba na timu hiyo, mkataba wenye thamani ya dola za kimarekani 25,000 kwa mwezi sawa na Tsh 57,975,000 kwa mwezi.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares