Michuano ya Jumatatu katika Bundesliga yafutwa

Baada ya kushuhudia upinzani mkali kutoka kwa baadhi ya wadau, na hasa mashabiki wa kandanda, hatimaze vilabu vya Ligi Kuu ya Kandanda Ujerumani – Bundesliga vimekubaliana kuifutilia mbali michuano ya Jumatatu kuanzia msimu wa 2021-2022.

Kitengo kinachosimamia Ligi ya Ujerumani – DFL kimethibitisha kuwa uamuzi huo ulifanywa kwa “kauli moja” katika mkutano ulioandaliwa Septemba. Mashabiki walikuwa wamesema kutakuwa na maandamano mapya katika michuano ya Novemba 30 hadi Desemca 3, ambayo ni ya kwanza msimu huu kujumuisha mtanange wa Jumatatu.

Mkataba wa sasa wa matangazo ya Bundesliga kwenye televesheni una michuano mitano ya Jumatatu kwa msimu lakini makubaliano yajayo sasa yatakuwa na mechi za ziada Jumapili. Mashabiki kila mara wanaelezea ghadhabu yao kuhusu michuano ya Jumatatu Ujerumani lakini katika ligi nyingine kuu, kama vile England, Uhispania na Italia, ni michuano inayochezwa kila mara Jumatatu

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends