Michuano ya Klabu Bingwa Afrika kutifua vumbi

17

Michuano ya hatua ya makundi kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika inarjea kesho Jumamosi katika mataifa mbalimbali. Katika kundi A, Lobi Stars ya Nigeria itamenyana na mabingwa watetezi Wydad Casablanca ya Morocco.

Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini nao watatifua na ASEC Mimosas ya Ivory Coast jijin Pretoria. Timu zote katika kundi hili, zina alama tatu, baada ya kushinda mechi moja. Mechi za makundi mengine zitachezwa siku ya Jumamosi, Februari 2.

Kundi B:-

FC Platinum vs Horoya

Orlando Pirates vs Esperance de Tunis

Kundi C:-

TP Mazembe ya DRC itaikaribisha Club Africain ya Tunisia. Kundi hili limesalia na klabu tatu, baada ya Ismaily ya Misri, kuondolewa kwa sababu ya mashabiki wake kuzua fujo katika mechi iliyopita dhidi ya Club Africain.

Kundi D:

AS Vita Club vs JS Saoura

Al-Ahly vs Simba

Author: Bruce Amani