Michuano ya robo fainali ya CAF yaanza

Michuano ya hatua ya robo fainali, kuwania Kombe la klabu bingwa – CAF Champions League na Shirikisho barani Afrika – CAF Confederation Cup, inachezwa mwishoni mwa juma hili.
Ijumaa usiku, Horoya ya Guinea itakuwa nyumbani kucheza na Al Ahly ya Misri huku ES Setif ikimenyana na Wydad Casablanca ya Morocco. Jumamosi kuanzia saa saa moja kamili saa za Afrika Mashariki, Primerio de Agosto ya Angola, itamenyana na TP Mazembe ya DRC. Mechi nyingine itachezwa saa nne usiku kati ya klabu kutoka nchi moja ES Tunis na Etoile du Sahel.

Jumapili, itakuwa ni zamu ya mechi za Shirikisho barani Afrika, CARA Brazaville ya Congo, itachuana na Raja Casablanca, Rayon Sport itakuwa jijini Kigali kucheza na Enyimba ya Nigeria, huku AS Vita Club ikicheza na RSB Berkane ya Morocco. Nayo Al Masry ya Misri itamenyana na USM Alger. Mechi hizi zinachezwa nyumbani na ugenini.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends