Migne aridhishwa na sare dhidi ya Ethiopia

50

Kocha wa Timu ya taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars, Sebastian Migne amesema ameridhishwa na pointi moja waliyopata katika mchezo wao wa mkondo wa kwanza dhidi ya Ethiopia siku ya Jumatano jijini Addis Ababa. Stars walitoka sare ya bila kufungana na Ethiopia na sasa inahitaji siku ya Jumapili kujiweka katika sehemu nzuri ya kufuzu katika fainali za mataifa ya bara Afrika AFCON mwaka 2019 nchini Cameroon.

Migne alisema kuwa mashabiki wa Ethiopia walifanya mchuano huo kuwa mgumu kwa Stars na akawaomba Wajenya kujitokeza kwa wingi ktika mechi ya marudiano jijini Nairobi. Matokeo ya Addis yameonekana kuwa mazuri kwa Kenya ambayo inaongoza kundi la F, nyuma ya Ethiopia ambayo pia ina alama nne. Ghana ni ya tatu kwa alama tatu, huku Sierra Leone ikiwa imefungiwa na Shirikisho la soka duniani FIFA.

Ethiopia pia ina nafasi ya kufuzu iwapo, itapata alama tatu muhimu dhidi ya Harambee Stars jijini Nairobi huku kocha wa nchi hiyo Abraham Mebartu akisema mechi hiyo itaamua hatima yao.

Kenya itamaliza mechi yake ya mwisho dhidi ya Ghana, mwezi Machi mwaka 2019 huku Ethiopia ikimalizia kibarua chake dhidi ya Ghana mwezi Novemba.

Mechi hizo za kufuzu zinaendelea:-

Alhamisi Oktoba 11. 2018

Congo vs Liberia

Ijumaa Oktoba 12. 2018

Cameroon vs Malawi
Gabon vs Sudan Kusini
Angola vs Mauritania
Nigeria vs Libya
Guinea vs Rwanda
Cote d’Ivore vs Jamhuri ya Afrika ya Kati
Misri vs Swaziland
Cape Verde vs Tanzania
Togo vs Gambia
Mali vs Burundi
Algeria vs Benin

Author: Bruce Amani