Misri yaungana na mataifa 6 wenyeji yalioondolewa mapema

Baada ya kipigo cha Afrika Kusini kwa wenyeji Misri hapo jana Jumamosi Julai 6 katika dimba la Kimataifa la Cairo sasa Mapharao wanaungana na timu nyingine sita wenyeji zilizoondoshwa hatua ya mtoano katika mashindano ya Afcon miaka ya nyuma.

Tangu kuanzishwa kwa mfumo mpya wa mashindano ya Afcon kuhusisha robo na nusu fainali zilikuwa hatua ya mtoano kwani kipindi hicho zilikuwa timu 8 pekee.

Timu zilikuwa 8 mpaka mwaka 1992 ambapo mfumo ulibadilika kidogo kwa kuongeza timu kufikia mataifa 12 ambapo hata hatua ya mtoano ikatokea, sasa tangu utaratibu huo kuanzishwa ni Mataifa 6 pekee yamewai kuandaa na kuondoshwa mapema katika hatua za awali.

Mbali na hivyo, Misri inakuwa timu ya kwanza mwenyeji kufungashiwa mizigo mapema kwenye Afcon

Orodha ya mataifa yaliyoandaa mashindano na kuondoshwa katika hatua ya mtoano ni pamoja na:-

1992 robo fainali Senegal 0-1 Cameroon.

2000 robo fainali Ghana 0-1 South Africa

2010 robo fainali Angola 0-1 Ghana

2012 robo fainali Equatorial Guinea 0-3 Cote d’Ivoire

2012 robo fainali Gabon 1-1 (4-5 pen.) Mali

2013 robo fainali Afrika Kusini 1-1 (1-3 pen.) Mali

2019 mkondo wa 16 bora Misri 0-1 Afrika Kusini.

Mwaka 2012, Equatorial Guinea na Gabon ziliandaa mashindano hayo kwa pamoja.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments