Mkongwe Tevez ajiweka kando Boca Juniors Argentina

Mkongwe Carlos Tevez ametangaza rasmi kuwa ataondoka katika klabu ya ujana wake ya Boca Juniors ya nchini Argentina ingawa hajaweka wazi kama ananuia kustaafu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37, kufuatia kuondoka kwake amesema damu yake ni Boca Juniors na sio katika klabu nyingine.
Tevez ambaye amewai kukipiga kunako klabu ya Manchester United, West Ham, Juventus na Manchester City hajathibitisha kama kuachana na Boca ni kwa ajili ya kustaafu au kwenda sehemu nyingine.
“Maisha yangu Argentina yamefikia ukomo, nilisema siwezi kucheza klabu nyingine zaidi ya Boca Juniors nchini. Ilikuwa fahari nitaendelea kujisikia furaha kucheza hapa”.
Tevez ambaye alimpoteza Baba mzazi mwezi wa pili kutokana na Covid-19 alisema hakupata muda wa mzuri wa kuomboleza

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares