Mkusanyiko wa matokeo ya EPL Jumamosi

54
Liverpool imeandika ushindi wa tano mfululizo wa EPL huku wakifikia rekodi ya Manchester City na Arsenal kwa kushinda mechi 14 mfululizo za EPL nyumbani wakati ambao wameitwanga goli 3-1 Newcastle United.
Jetro Willems alianza kuiandikia goli Newcastle kabla Sadio Mane kufunga goli mbili na Mohamed Salah akafunga idadi ya magoli katika mchezo huo
Manchester City imeangukia pua baada ya kukubali kipigo cha goli 3-2 katika mchezo ambao City walikuwa ugenini. Unakuwa mchezo wa pili kwa Manchester City kuvutwa shati ndani ya msimu huu. Goli za Kun Aguero na Rodri hazikusaidia kufuta goli la Pukki, Cantwell na McLean ya Steven Bruce.
Tottenham ikiwa inajiandaa na Ligi ya Mabingwa kama ilivyo kwa Liverpool, Chelsea, City imeibuka na ushindi wa goli 4-0 dhidi ya Crystal Palace katika mchezo wa nyumbani, White Line.
Son akifunga goli 2, Lamela goli moja na lingine la kujifunga likifungwa na Van Aanholt.
Burnley imepata alama kwa Brighton.
Kinda Tammy Abraham amefunga goli tatu katika mchezo dhidi ya timu ngumu ya Wolverhampton Wanders kwa kushinda goli 5-2 ikiwa ni hat-trick yake ya kwanza ndani ya The Blues.
Kinda mwingine Mount amefunga goli moja, Tomori moja huku Abraham baada ya kufunga tatu akawa amejifunga moja katika harakati za kuoko michomo na Cutrone wa Wolves akifunga moja.

Author: Bruce Amani