Mkusanyiko wa matokeo ya EPL Jumamosi

Manchester City imeanza kuwania taji la tatu mfululizo kwa kuifumua West Ham United goli 5-0 katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi kuu ya England uliopigwa nyumbani kwa West Ham leo Jumamosi.
Matumizi ya VAR yametumika kwa kiasi kikubwa katika kutoa ushindi wa City huku Raheem Sterling akionekana kunufaika nako baada ya kufunga goli tatu, Gabriel Jesus na Sergio Aguero wote wamefunga goli moja.
TOTTENHAM
Harry Kane amefunga mara mbili katika dakika 4 za mwisho baada ya Aston Villa kutaka kuibuka na ushindi ndani ya dimba la Tottenham. Spurs, walimaliza nafasi ya nne msimu uliopita goli lake la kwanza limefungwa na saini mpya Tanguy Ndombele.
SHEFFIELD UNITED
Imetosha nguvu na Bournemouth kwa sare ya goli 1-1. Hii inakuja baada ya kupanda daraja msimu huu huku mara ya mwisho ilikuwa miaka 12 iliyopita.  Billy Sharp akifunga dakika ya 88 ya mchezo akisawazisha goli la Chris Mepham.
EVERTON
Usajili mkubwa umeshindwa kufanya kazi kwa vijana wa Rogers. Ingizo jipya kutoka Arsenal Alex Iwobi, Moise Kean kutoka Juventus hola mbele ya Crystal Palace suluhu yakamilisha mchezo huo.
Mlinzi wa Everton Morgan Schneiderlin alitupwa nje kwa kadi nyekundu huku winga wa klabu ya Crystal Palace Wilfred Zaha akianzia bechi na kuingia dakika ya 76 ikiaminika kuyokuwa sawa baada ya dirisha la usajili kufungwa.
BRIGHTON 3-0 WATFORD
Iliingia kwenye mchezo huo wakiwa na kocha mpya Potter Graham. Iliingia kwenye dimba la Vicarage, Watford ikiwa haijapata ushindi kwenye mechi tano kati ya saba.
Kesho Jumapili ni Frank Lampard dhidi ya Ole Gunnar (OGS) dimba la Old Trafford saa 18:00 jioni.
Kabla ya hapo kutakuwa na Newcastle United dhidi ya Arsenal saa 16:00.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends