Mkusanyiko wa patashika ya usajili wa wachezaji EPL

63

Dirisha kubwa la usajili England limefungwa rasmi leo Ijumaa baada ya kudumu kwa takribani siku 30 na zaidi huku kila timu ikifanya usajili wa wachezaji na timu nyingine zikiuza wachezaji.

Amani Sports News inakuleta majina ya wachezaji walioingia au kutoka katika klabu husika.

EVERTON

Klabu hii imefanya usajili mkubwa sana msimu huu, imekubali kutoa pauni milioni 34 kwa Alex Iwobi kutokea nchini Arsenal.

Wachezaji wengine walioingia Goodson park ni pamoja na Moise Kean kutokea Juventus, Andre Gomes, Fabian Delph, Jonas Lossl na Djibril Sidiba.

ARSENAL

The Gunners imetumia pesa zaidi dirisha hili hasa katika siku ya mwisho la kufungwa kwa dirisha hilo. Wachezaji walioingia:- Nicolas Pepe kutoka Lille, Gabriel Martinelli, Dani Ceballos, William Saliba, Kieran Tierney na David Luiz kutoka Chelsea pauni milioni 8.

MANCHESTER UNITED

Zaidi ya asilimia 80 ya wachezaji waliohusishwa na timu hiyo watatu tu ndio wamefanikiwa kujiunga na timu hiyo. Wachezaji walioingia ni:- Harry Maguire, James Daniel na Aaran Wan-Bissaka.

MANCHESTER CITY

Tofauti na miaka mingine, City mwaka huu imesajili wachezaji watano tu, Rodri, Angelino, Zack Steffern, Joan Cancelo na Scott Carson.

LIVERPOOL

Haijatoa mchezaji yeyote kwenye kikosi cha kwanza na haijasajili mchezaji atakaeingia kikosi cha kwanza. Wachezaji walioingia ni makinda :- Sepp Van Berg, Harvey Elliot na Andrian.

LEICESTER CITY

Mbweha hawa wamefanikiwa kusajili wachezaji wanne tu, Youri Tielemans, Ayozo Perez, James Justin na Vontage Campbell.

TOTTENHAM HOTSPURS

Vijana wa Pochettino walifanya vizuri msimu uliopita bila kufanya usajili hata mmoja wakifika fainali ya Uefa, msimu wa 2019/20 imeingia benki na kutoa pesa kwa Tanguay Ndombele, Ryan Sessegson, Jack Clarke na Lion Etete.

Wachezaji waliondoka:- Romelu Lukaku amejiunga na Inter Milan, Luiz ajiunga na Chelsea, Kiungo wa Chelsea Drinkwater amesajiliwa na Watford

Timu zote EPL zimehusika katika usajili msimu huu na katika hali ya kushangaza msimu wa 2018/2019 usajili mkubwa ulifanyika hali kadhalika kwa msimu huu majina mengi ya wachezaji wametoka timu moja kwenda nyingine katika siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

Zaidi ya pauni bilioni 1.41 zimetumika katika usajili kwa msimu huu kwa vilabu vyote vya EPL huku klabu ya Arsenal ikiingia kama timu iliyotumia pesa kubwa zaidi katika usajili wa wachezaji sita.

Author: Bruce Amani