Mkuu wa WHO Tedros aunga mkono Michezo ya Olimpiki

Mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni – WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema leo kuwa Michezo ya Olimpiki inapaswa kuendelea kama ilivyopangwa ili kuudhirishia ulimwengu kile kinachoweza kufanywa wakati kukiwa na mpango na hatua sahihi wakati huu wa janga la COVID-19. Akiwahutubia wanachama wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki – IOC katika kikao chao mjini Tokyo, Japan, Tedros amesema ulimwengu unahitaji kwa sasa Michezo ya Olimpiki kama “sherehe ya matumaini”.

Amesema michezo ya Olimpiki ina nguvu ya kuuleta pamoja ulimwengu, kutia moyo na kuonyesha kinachowezekana. Michezo hiyo ya Tokyo inaanza Ijumaa 23 Julai wakati kukiwa na maswali kuhusu usalama kutokana na kitisho cha maambukizi ya virusi vya corona, ambapo maelfu ya wageni wanawasili nchini humo.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares