Mmiliki wa Manchester United Glazer achutama kwa mashabiki United

1,021

Mmiliki mweza wa klabu ya Manchester United Joel Glazer amepanga kufanya majadiliano rasmi na mashabiki wa timu hiyo ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuingia kwenye umiliki mwaka 2005.

Familia ya Glazer imekuwa ikitoa taarifa mbalimbali juu ya mwenendo wa klabu hiyo kama mashabiki kuingia uwanjani Jumapili tukio lililopelekea kufutwa kwa mchezo wa Manchester United dhidi ya Liverpool.

Katika barua ya Glazer, aliwaomba radhi wachezaji, viongozi na mashabiki kutokana na wamiliki hao kukubali kujiunga na European Super League.

Akisema “tunahitaji kuwa wamoja kama asili ya klabu yetu, tukiwa na miiko inayotuongoza na tamaduni zetu, ndiyo tunataka mabadiliko lakini yanayowahusisha mashabiki” alisema.

Kwa uelewa mpana, ni kuwa barua ya Glazer ni kulainisha mioyo ya mashabiki, kuruhusu kuzungumza ni kuonyesha wako tayari ambapo pia barua hiyo ni alama kuwa wako tayari kubadilika kama matakwa ya mchezaji wa 12.

Majadiliano hayo rasmi yanakusudiwa kufanyika mara tu msimu huu utakapomalizika.

United watacheza na Villarreal katika fainali ya Ligi ya Europa Mei 26, na inafahamika kuwa kikao hicho kitafanyika baada ya mtanange huo.

Author: Bruce Amani