Mo Farah apanga kurejea katika mbio za mita 10,000

Mshindi wa medali ya dhahabu katika michezo ya Olimpiki Mo Farah ametagaza kuwa atarejea katika mashindano ya mbio za mita 10,000 mwaka ujao katika jaribio la kushinda taji la tano la Olimpiki mjini Tokyo.

Mwanariadha huyo wa mbio ndefu Muingereza alitundika njumu zake za kushiriki mbio za ndani ya uwanja mwishoni mwa 2017 baada ya mashindano ya ubingwa wa Dunia mjini London, ambko alishinda taji lake la sita la dunia kwa kushinda mita 10,000 na kunyakua fedha katika mita 5,000.

Aligeukia mbio za barabarani mwaka wa 2018, akimaliza wa tatu katika London Marathon na kisha akashinda Chicago kwa kuweka rekodi ya Ulaya ya 2:05:39.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends