Mo Salah ahifadhi tuzo ya CAF ya mchezaji bora wa mwaka

185

Mohamed Salah, amempiku mwenzake wa Liverpool Sadio Mane na kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2018. Salah ameshinda tuzo hiyo kwa mwaka wa pili mfululizo. Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Gabon pia alikuwa kwenye orodha ya wachezaji watatu waliowania tuzo hiyo.

Salah, mwenye umri wa miaka 25, aliweka historia kwa kuwa Mmisiri wa kwanza kutwaa taji hilo tangu lilipoanzishwa mwaka wa 1992. Ni mara yake ya pili kuwa katika orodha ya majina matatu bora. Analenga kujiunga na orodha ya wachezaji waliotwaa mara mbili mfululizo. El Hadji Diouf wa Senegal (2001,2002), Samuel Eto’o wa Cameroon (2003, 2004) na Toure (2011, 2012).

Muafrika Kusini Chrestinah Thembi Kgatlana ndiye mshindi wa tuzo hiyo kwa upande wa wanawake. Mfaransa Herve Renard amebeba tuzo ya kocha bora kwa wanaume. Anainoa timu ya taifa ya Morocco

Author: Bruce Amani