Molinga asajiliwa Namungo FC

Namungo FC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara imekamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo David Molinga akitokea Zambia katika klabu ya Zesco United.

Molinga maarufu kama “Papaa” anajiunga na Namungo FC ikiwa ni miaka miwili pekee imepita tangia mchezaji huyo kuondoka Yanga iliyokuwa chini ya kocha Mwinyi Zahera.

Namungo imeweka kambi Lindi ikiwa na hesabu za kufanya vema msimu ujao wa 2021/22 kwa mujibu wa kocha mkuu Hemed Morocco.

Pia nyota mwingine wa kigeni ambaye yupo ndani ya Namungo Fc ni pamoja na Obrey Chirwa ambaye alikuwa anachezea Yanga kabla ya Azam FC msimu uliopita.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares