Morata aisaidia Atletico kuwawekea shinikizo vinara Barcelona

Atletico Madrid wameendelea kuwafukuzia vinara wa La Liga Barcelona baada ya mabao mawili ya Alvaro Morata yakiwapa ushindi wa 2 – 0 dhidi ya Real Sociedad Jumapili, licha ya kucheza kucheza nusu saa katika kipindi cha pili na wachezaji 10 baada ya Koke kutimuliwa uwanjani.

Morata, ambaye alifunga bao lake la kwanza akiwa na Atleti katika ushindi wao wa wiki iliyopita wa 2 – 0 dhidi ya Villarreal, alifunga bao la kichwa na dakika tatu baadaye tena akaruka juu na kusukuma wavuni mpira.

Atletico wako katika nafasi ya pili kwenye jedwali la La Liga na pointi 53, tano mbele ya nambari tatu Real Madrid, na saba nyuma ya vinara Barca, ambao wana pointi 60 baada ya ushindi wao wa 1 – 0 dhidi ya Real katika Clasico ya Jumamosi.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends