Morocco taifa la kwanza kusimamisha michezo kutokana na COVID-19

Shirikisho la Mpira wa Miguu Morocco limesitisha shughuli zote za kimichezo nchini humo mpaka watakapotoa taarifa nyingine. Hii ni kutolana na hofu ya Virusi vya Corona.

FRMF ambalo ni Shirikisho nchini humo limesema kuwa katazo hilo litayaathiri mashindano yote bila kujali umuhimu wake.

Maamuzi hayo yanakuja katika kipindi ambacho tayari kumeripotiwa matukio ya watu 17 kukutwa na virusi hivyo sambamba na kifo cha mtu mmoja.

“Kuanzia sasa tunasitisha michezo yote ya mpira mguu sawa na aina nyingine ya michezo kutoka siku ya tangazo hili,” ilisema taarifa hiyo kupitia mtandao wa kijamii wa Shirikisho hilo.

Aidha, katazo hilo linakuja siku moja baada ya Wizara ya michezo kuzuia shughuli zote za michezo nchini humo.

Mtanange wa Raja Casablanca dhidi ya Ismaily wa Kombe la Mataifa ya Urabu uliopagwa kuchezwa Jumapili hii hautachezwa ikiwa ni sehemu ya athari ya katazo la serikali sambamba na FRMF.

Ugonjwa wa virusi vya Corona, unaambukizwa kwa hewa ambapo dalili zake ni kama kukohoa, na kupumua kwa shida, kukosa hamu kula, mpaka sasa umeenea kwa kiwango kikubwa ambapo zaidi ya watu 116,000 wameathirika na Virusi hivyo duniani.

Wanasayansi wamethibitisha kuwa ugonjwa huo unahitaji siku tano pekeee kuonyesha dalili zake.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends