Morrison ashinda kesi CAS

Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo ‘CAS’ imetangaza hukumu ya Kesi iliyofunguliwa na klabu ya Young Africans mwaka mmoja uliopita dhidi ya Kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ghana Bernard Morrison.

Majibu ya hukumu ya Kesi hiyo iliyochukua muda wa mwaka mmoja na zaidi, yametangazwa Novemba 23 majira ya jioni, ambapo Mchezaji Morrison ameshinda.

Hata hivyo CAS imeitaka klabu ya Young Africans kumlipa fidia Morrison ya Shilingi Milioni 12.

Young Africans walifungua kesi hiyo, baada ya kutokuyakubali maamuzi yaliyotangazwa na Kamati ya Hadhi za Wachezaji ya TFF ambayo ilimuidhinisha Morrison kuwa mchezaji huru mwaka 2020, kufuatia mvutano wa kimkataba uliokuwepo baina ya pande hizo mbili.

Hatua ya kuachwa huru, ilimuwezesha Morrison kujiunga na Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, ambao bado anawatumikia hadi sasa.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends