Mourinho asema atakumbukwa kwa mazuri mengi Tottenham

Jose Mourinho ni kama ameanza kutabiri safari ya kuondoka kwake klabuni Tottenham Hotspur baada ya leo kusema kuwa anaamini atakumbukwa kwa mema aliyoyafanya ndani ya klabu hiyo ya London.

Anaamini atakumbukwa kwa mazuri na sio mabaya.

Siku za karibuni kumeibuka tetesi kuwa klabu ya Spurs ipo sokoni kusaka nafasi ya kocha mkuu mpya baada ya kwenda mechi sita za Ligi Kuu nchini England bila ushindi.

Kipigo cha goli 2-1 dhidi ya West Ham United siku ya Jumapili kilikuwa kinaiacha Spurs nafasi ya tisa kwenye msimamo wa EPL wakati West Ham wakipanda mpaka nafasi ya nne bora.

“Najua kuna siku nitaondoka hapa, lakini naamini hata nikiondoka nitakumbukwa mema, na sio mabaya” alisema Mourinho ambaye kikosi chake kitashuka uwanjani kesho Jumatano kwenye mechi ya Ligi ya Europa.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares