Mtibwa Sugar yanasa saini ya Ndemla wa Simba

Mtibwa Sugar imemtambulisha rasmi kiungo mshambuliaji wa Simba Said Ndemla kuwa mali yao kwa msimu mmoja kandarasi ya mkopo.

Ndemla anajiunga na Mtibwa Sugar baada ya kutumika Simba kwa muda mrefu ingawa nafasi yake ya moja kwa moja ikiwa hafifu katika kikosi hicho.

Mtibwa Sugar ambayo inatarajiwa kuwa chini ya Kocha Mkuu, Hitimana Thiery huu unakuwa ni usajili wake wa kwanza kuutambulisha kwa mashabiki wake baada ya dirisha kufungwa Agosti 31.

Msimu uliopita, Mtibwa Sugar iliponea chupu chupu ya kushuka daraja kabla ya kocha Mohammed Badru dakika za jioni kuipa usalama na uhakika wa kucheza TPL msimu 2021/22.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares