Mtu mmoja amekatwa baada ya kumtolea maneno ya kibaguzi Rio Ferdinand

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Jamie Arnold mwenye umri wa miaka 31, amekatwa na Jeshi la Polisi la West Midlands kufuatia kutuhumiwa kutoa maneno ya kibaguzi pamoja na matusi kwa mchezaji wa zamani wa Manchester United na Mchambuzi wa Kandanda Ulaya Rio Ferdinand.

 

Jamie Arnold alitoa lugha ambayo sio nzuri kwa Rio Ferdinand katika mchezo wa Manchester United dhidi ya Wolves uliopigwa Mei 23, ilibainisha taarifa ya Polisi Magharibi ya Midlands.

 

Pia, mtu huyo kutokea Stone, Staffordshire, anatuhumiwa kutua lugha yenye viashiria vya chuki kwa rio Ferdinand.

 

Mr Arnold ana nafasi ya kupinga/kukataa rufaa Mahakamani Julai 29, 2021.

 

Alikamatwa wakati mechi ikiendelea, na ilikuwa mechi ya kwanza mashabiki kurejea viwanjani baada ya kuzuiliwa na Serikali kutokana na janga la Covid-19 mtanange uliopigwa dimba la Molineux.

 

Ferdinand alitupia maneno kwenye Twitter yake juu ya kitendo hicho, ambapo Manchester United waliibuka washindi kwa bao 2-1.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares