Mugisha kutamba katika mashindano ya dunia

Mshindi wa mbio za baiskeli za Tour Du Rwanda Samwel Mugisha amesema amejipanga kuhakikisha anafanya vyema katika michuano ya baiskeli ya dunia itakayofanyika mwishoni mwa mwezi huu nchini Austria. Mwendesha baiskeli huyo ataiwakilisha timu ya Rwanda katika mashindano hayo yanayotazamiwa kuanza Septemba 22 hadi Septemba 30.

Waendesha baiskeli wengine watakaoiwakilisha Rwanda katika michuano hiyo ni Didier Munyaneza, Jean Paul Ukiniwabo na Joseph Areruya

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends