Muguna ajiunga tena na Gor

Mabingwa wa ligi kuu ya kandanda Kenya KPL Gor Mahia wamethibitisha kumsaini tena kiungo Kenneth Muguna kwa mkataba wa miaka mitatu.

Muguna anajiunga tena na mabingwa wa ligi baada ya kuhamia klabu ya Tirana nchini Albania mwaka wa 2017.

Muguna, ambaye alipigiwa kura kuwa mchezaji mwenye thamani kubwa zaidi katika ligi ya KPL mwaka wa 2016, alijiunga kwa mara ya kwanza na Gor Mahia akitokea Wester Stima mwaka wa 2017 na akachangia pakubwa katika kuisaidia Gor Mahia kunyakua tena taji la ligi kutoka kwa Tusker FC mwaka huo kwa kufunga mabao matatu kwenye ligi.

Ni mchezaji wa pili kusainiwa na mabingwa hao katika kipindi hiki cha uhamisho baada ya beki wa timu ya taifa ya Uganda Shafik Batambuze kutia wino mkataba na mabingwa hao wa Kenya kwa mara ya 17.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends