Mukoko Tonombe akanusha uvumi wa kwenda Kaizer Chiefs

Kiungo mkabaji wa klabu ya Yanga, Mukoko Tonombe amekanusha taarifa za kufanya mazungumzo na klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo kufuatia siku za karibuni kuwepo kwa taarifa ya kuhitajika.

Tonombe baada ya kusajiliwa na Yanga akitokea AS Vita na kuonyesha kandanda safi kwa kipindi chote hicho, tetesi zilianza kuibuka kuwa mchezaji huyo anayekitumikia pia kikosi cha timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anahitajika na wababe hao wa soka la Afrika Kusini.

Awali taarifa za kuhitajika kwake zilikuwa zikimhusisha pia winga wa klabu hiyo hiyo ya Yanga Tuisila Kisinda ingawa baadaye Yanga kupitia Afisa Habari Hassan Bumbuli walikanusha taarifa hizo, kuwa sio kweli.

Hata hivyo, baada ya Tonombe Mukoko kurejea kutoka kwenye majukumu ya timu ya taifa akizungumzia tetesi hizo mbele ya Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam amesema hazina ukweli kwani yeye bado anakandarasi na Yanga.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares