Mwakinyo Achapwa na Smith kwa TKO

212

Hassan Mwakinyo, Bondia wa Kitanzania ameshindwa kufurukuta mbele ya Muingereza, Liam Smith baada ya kupigwa kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya nne ukumbi wa M&S Bank Arena Jijini Liverpool, England.

Mwakinyo ambaye awali alitengenegeza matumaini makubwa kwa watanzania kutokana na kushinda mataji mengi ya nyumbani ingawa hata hapo Uingereza mwaka 2018 alishinda pambano moja ambalo lilimtambulisha vyema.

Baada ya kufungwa, Hassan Mwakinyo alitumia mitandao yake ya kijamii kuomba msamaha kwa wapenzi wake na watanzania kwa ujumla

“Najua nimewaamuzi wengi nami pia sipendi kupoteza katika maisha yangu, nilibadilishiwa vifaa siku ya pambano kwa kuwa nilipewa viatu ambavyo sijawahi kufanyia mazoezi jambo ambalo lilinifanya nimwambie mwamuzi kuwa nina maumivu kwenye enka.

“Mara ya pili ilikuwa hivyo lakini mwamuzi hakuweza kunisikiliza na kuamua kumpa ushindi mpinzani wangu, sijapenda katika hili ninaomba msamaha,” amesema Mwakinyo.

Author: Asifiwe Mbembela