Mwakinyo afuta machozi ya Taifa Stars kwa Watanzania

Bondia Hassan Mwakinyo amefanikiwa kushinda pambano lake dhidi ya mpinzani kutokea Argentina Jose Carlos Paz katika mpambano uliofanyika leo Ijumaa Jijini Dar es Salaam.
Ushindi wa Hassan Mwakinyo ambaye alikuwa anatetea mkanda wake wa WBF Intercontinental Super Welterweight unamaanisha ataendelea kuushikilia pengine hadi mwakani 2021. Bondia huyo mkazi wa Tanga amempiga Paz kwa TKO raundi ya nne.
Kupitia ukurasa rasmi wa Twitter wa bondia huyo ameandika kuwa “Ushindi Wangu Wa Leo ni Maalumu kwa Taifa Langu, Natamani Ushindi Huu Ukawe Mfano Kwa Mabondia Wengine Nawashukuru Sana Watanzania Kwa Sala, Dua Na Sapoti  zenu Katika Kufanikisha Hili” 🇹🇿
Mbali na mpambano huo, pambano lingine lililovutia katika usiku wa vitasa ni pale akina mama walipoingia ulingoni kuonyesheana ubabe, ambapo bondia Mkenya Fatuma Zarika ametwaa ubingwa wa WBF (Kg 57) baada ya kumchapa Mzimbabwe Patience Mastara kwa pointi.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares