Mwakinyo atetea taji la ABU kwa kumbwaga sakafuni Mnamibia

Bondia wa Kitanzania Hassan Mwakinyo, amefanikiwa kutetea ubingwa wake wa Afrika ABU katika pambano la uzito wa Super Welterweight baada ya ushindi kwa TKO katika raundi ya nne.

Ilikuwa ni dhidi ya bondia Julius Idongo kutoka Namiba kwenye mchezo wa Mabingwa wa Ulingo uliochezwa usiku wa kuamkia Leo Jumamosi katika ukumbi wa Ubungo Plaza Dar es Salaam.

Ilikuwa ni katika pambano la raundi 12, Mwakinyo alishinda katika raundi ya nne na kumfanya aweze kutetea taji lake.

Baada ya ushindi huo Mwakinyo amesema kuwa ushindi huo ni kudra za Mungu na anashukuru kwa kushinda.

Kwa upande wa Mnamibia Idongo amesema kuwa haelewi imekuajekuaje akashindwa katika pambano hilo kwa kuwa anaamini katika uwezo wake.

Hassan Mwakinyo ameendelea kupeperusha vyema bendera ya Tanzania, huku ubora wake ukionekana kusimama kila leo tangia pambano lake la England miaka miwili nyuma.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares