Mwalimu Kashasha afariki dunia

Shirika la Utangazaji Tanzania TBC limethibitisha kifo cha aliyekuwa Mchambuzi nguli wa kandanda nchini Mwalimu Alex Kashasha ambaye umauti umemfika akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Kairuki Jijini Dar es Salaam

Kwa mjibu wa taarifa hiyo inasema Mwalimu Kashasha alipoteza maisha saa 9 alasiri.

Kashasha alikuwa amelazwa Hospitalini hapo wiki mbili zilizopita ambapo kazi yake ya mwisho ilikuwa kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho Kigoma baina ya Simba na Yanga.

Kwa taarifa za awali zinasema marehemu amefariki kwa tatizo la figo lililopelekea kulazwa hospitalini hapo na sasa wanapanga taratibu za maziko.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends