Mwamnyeto atua Yanga Dirisha la Usajili likifunguliwa Bongo

576

Baada ya Dirisha la Usajili kwa Klabu za Ligi Kuu Tanzania, Ligi daraja la kwanza (FDL), Ligi Daraja la pili (SDL) na Ligi Kuu ya Wanawake kufunguliwa rasmi Agosti , 2020 vilabu mbalimbali vya VPL nchini vimeanza kufanya usajili kujipanga na msimu ujao ambapo Simba, Yanga na Azam zimekuwa za kwanza kuvuta majembe mapya kwa ajili ya msimu wa 2020/21.

Haya hapa ni majina ya majembe hayo kwa kila klabu;

Klabu ya Azam ambayo kupitia Msemaji wake Thabit Zakaria “Zaka Zakazi” alinukuliwa na vyombo vya habari akisema timu hiyo itafanya usajili wa majina 15 ya wachezaji wa ndani na nje ya Tanzania.

Ally Ramadhani Niyonzima (kiungo Mkabaji wa Kimataifa wa Rwanda), Ayoubu Lyanga (Winga wa Coastal Union), Awesu Awesu (Kiungo wa Kagera Sugar) ni miongoni mwa wachezaji ambao tayari wameshasajiliwa Azam Fc kati ya wale kumi na tano.

Bakari Nondo Mwamnyeto (Beki wa Kati wa Coastal Union), Zawadi Peter Mauya(Kiungo Wa Kagera Sugar), na Yassin Mustapha Salum( Beki wa Kushoto wa Polisi Tanzania) ni wachezaji ambao wamekamilisha usajili katika kikosi cha Young Sports Club.

David Kameta ‘Duchu’ ni mchezaji pekee ambaye amesajiliwa katika kikosi cha Simba Sports Club akitokea Lipuli Fc.

Mwezi mmoja pekee ndio ambao umetolewa na mamlaka husika katika usajili ili kukimbizana na ufinyu wa muda wa maandalizi ya ligi kuu kwa msimu ujao huku baadhi ya wachambuzi wa soka nchini Tanzania wamelalamikia ufinyu wa muda kwa vilabu vidogo.

Author: Asifiwe Mbembela