Mwanamichezo wa Uganda aingia mitini kuelekea Michezo ya Tokyo 2020

329

Kamati ya Olympiki ya Uganda (UOC) imethibitisha kuwa mchezaji wao mmoja amekimbia kambini na kuelekea kusikojulikana wakati timu ya Uganda ikijiandaa na Michezo ya Olympiki Tokyo 2020.

 

Mazoezi hayo ya Uganda yalikuwa yanafanyika Japan katika Mji wa Osaka ambapo Uganda ilitegemea kushiriki kwenye michezo kadhaa.

 

Timu nzima ya Uganda iliyokuwa imeambatana na Viongozi, Wanandondi, Waogeleaji na Mnyanyua Vyuma (Weightlifter) walikuwa na maandalizi katika eneo la Izumisano, Osaka, Japan tangia tarehe za mwishoni mwa mwezi Juni kabla ya kuanza kwa michuano hiyo rasmi Julai 23.

 

Katika taarifa ya Kamati ya Olympiki Uganda ilibainisha kuwa, aliyekimbia kambini ni Mnyanyua vyuma anayefahamika kwa jina la Julius Sekitoleko.

 

“Tulitegemea angefuzu vipimo vya Covid-19, hata hivyo hakutokea kama alivyokuwa amearifiwa mapema ya Shirikisho la Wabeba Vitu-Vizito Kimataifa Julai 5, 2021”, ilisema taarifa ya UOC.

 

“Hivyo alitakiwa yeye (Sekitoleko) na kocha wake walikuwa wanategemewa kurudi Uganda kesho Jumatatu Julai 20”.

 

Matokeo ya kuingia mitini kwa mchezaji huyo kunaendeleza ugumu wa timu iliyoenda Japan ya Uganda, awali wachezaji wawili walitakiwa kuingia hatua ya kujitenga wenyewe kufuatia kubainika kuwa na viashiria vya Covid-19.

Author: Bruce Amani